The House of Favourite Newspapers

Diamond Amlipia Tiffah Milioni 50

0

DIAMOND Platinumz ni staa mkubwa wa muziki barani Afrika; ni staa mwenye wafuasi wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii kwa ukanda wa Afrika Mashariki hivyo hana jambo dogo kwa kuwa kuna vijana wengi wanamtazama yeye kama mfano.


Diamond ni mwimbaji,
dansa, mwandishi wa nyimbo, mfanyabishara, balozi wa brandi mbalimbali na baba wa watoto wanne wanaojulikana.


Diamond amejikuta akipagawa
baada ya mwanawe wa kwanza na wa kike pekee aliyezaa na mwanamama tajiri wa Uganda, Zari The Boss Lady, Tiffah Dangote alipohitimu shule ya awali na sasa amekwenda darasa la kwanza.


Januari 11, mwaka huu, Tiffah
mwenye umri wa miaka sita, alihitimu darasa la awali aliloshindwa kuhitmu mwaka jana kwa sababu ya kufungwa kwa shule nchini Afrika Kusini kutokana na janga la UVIKO-19.


Tiffah alihitimu katika shule
ya kishua ya matajiri inayoitwa Crawford International Pretoria Preparatory nchini Afrika Kusini. Diamond alifurahishwa na ishu hiyo kiasi cha kumuandikia; Najivunia moyo wangu…”


Kitu pekee ambacho gazeti hili
linakijua ni kwamba, Diamond au Mondi anampenda mno Tiffah kuliko viumbe wengine ndiyo maana binti huyo ndiye ametajwa mara nyingi zaidi kwenye nyimbo za jamaa huyo.


Tiffah anaendelea kusoma
kwenye shule hiyo ya kifahari ambapo kwa muijibu wa tovuti yake, Diamond analazimika kumlipia Tiffah ada inayokadiriwa kufikia shilingi milioni 50 za Kibongo kwa mwaka mmoja. Baada ya kufuatilia kiasi hicho cha ada anayolipiwa Tiffah, baadhi ya wafuasi wa Diamond vichwa vimepata moto na kuwa na maoni tofautitofauti.


Baadhi yao wanaunga mkono
wakisema anastahili kulipiwa mamilioni kama hayo na zaidi kwa kuwa Diamond ana uwezo na binti yake huyo ni mtoto staa zaidi Afrika.


Watoto wengine wa Diamond
ni Prince Nillan ambaye naye amezaa na Zari kisha Dyllan aliyezaa na Hamisa Mobeto ambao wapo darasa la awali (baby class) huku Naseeb Junior aliyezaa na Tanasha Donna akiwa bado hajaanza kwenda shule.

STORI; SIFAEL PAUL, DAR

Leave A Reply