The House of Favourite Newspapers

Diamond Aripoti Polisi

Diamond na maafisa wa polisi

MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz leo Februari 15, 2015 amejisalimisha kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga na kufanyiwa mahojiano kuhusu kuendesha gari  kwa kasi huku akicheza muziki.

Global Publishers imemtafuta Kamanda Mpinga na haya ndiyo majibu yake

“Ni kweli Diamond ameripoti kwetu leo, tumemhoji lakini amekiri kosa la kuvunja sheria za barabarani kwa kuendesha gari huku akicheza muziki ili hali akijua kuwa ni kinyume na sheria za nchi.

“Kwa sababu sheria ziko wazi, na mtuhumiwa amekiri kosa tumempiga faini ya shilingi elfu sitini (TZS 60,000) na kumuachia huru.” Kamanda Mpinga alisema.

Diamond amejisalimisha kituoni hapo kufuatia video yake kusambaa mitandaoni wiki iliyopita ikimuonesha akiendesha gari huku akicheza muziki sambamba na familia yake ambamo alikuwemo mama yake mzazi, Sandra, mpenzi wake Zari pamoja na watoto wao na ndugu wengine. Ikumbukwe kuwa baada ya tukio hilo Kamanda Mpinga alimtaka Diamond afike Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani kwa ajili ya kutoa maelezo.

Taarifa zaidi endelea kufuatilia hapa.

 

Comments are closed.