The House of Favourite Newspapers

Diamond: Wema amemharibu Tiffah

0

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’

Musa mateja

Kila kitu ukizidisha ni sumu! Ndivyo ilivyotokea kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye anadaiwa kumtupia lawama mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuwa amemharibu mtoto wao, Latifah Nasibu ‘Princes Tiffah’ kwa kumzidishia vikorombwezo vya urembo, Ijumaa Wikienda limetonywa.

 Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.

Habari kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho ni ‘memba’ wa familia ya Diamond au Dangote au Chibu zilieleza kwamba, kitendo cha Zari kumpodoa Tiffah kupita kiasi kimekuwa kikimpa shaka jamaa huyo akihofia kuwa kinaweza kumsababishia mwanaye kilema.

“Unajua mwanzoni Zari alianza kwa kumpaka lipstick na kumchora wanja lakini Diamond hakuona ni ishu sana.“Lakini Zari alipoanza kumwekea mawigi na kope za bandia, ndiyo jamaa akashtuka na kuanza kuuliza kama zina madhara au hazina?

“Kila Zari akitupia picha za Tiffah kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram zikimuonesha akiwa na mawigi na kope bandia ndivyo maoni ya watu yanazidi kuwa mengi wakimponda kuwa anamharibu mtoto wa Diamond.

“Daktari alimweleza kope bandia huongeza uzito kwenye misuli ya kope halisi, matokeo yake huifanya misuli ilegee na kuna uwezekano wa mbandikaji au mbandikwaji akawa kipofu japokuwa madhara hayo hayawezi kuonekana ndani ya muda mfupi,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

Kufuatia ishu hiyo, Diamond amekiri kuwasiliana na Zari ambaye amemtoa hofu kwamba ni mambo ya kutengeneza kwenye kompyuta siyo vikorombwezo vya kweli.

Leave A Reply