The House of Favourite Newspapers

Dida Amrudia Mungu… Aangushiwa Dua Saa Chache Baada ya Kunusa Kifo

0

 

KUFUATIA kuandamwa na mikosi kila kukicha huku akidai kunusurika kifo, mtangazaji mwenye jina kubwa Bongo, Khadija Shaibu ‘Dida’ anayekimbiza na kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani cha Radio Times FM ya Dar, wiki iliyopita aliamua kumrudia Mungu wake baada ya kuchomewa ubani kasha kuangushiwa dua maalum.

Katika tukio hilo lililoshuhudiwa na Wikienda, Dida alifanyiwa dua hiyo kwa zaidi ya dakika 30 na Shehe wa Msikiti Mkuu wa Morogoro, Alhaj Masenga.

Kwa mujibu wa Dida, alifi kia uamuzi huo wa busara baada ya kunusurika kifo maeneo ya Maseyu Mikese alipokuwa akitokea Dar kuelekea Morogoro kwenye shughuli ya maulid iliyoandaliwa na mdogo wake, Warda Makongwa ambaye naye ni mtangazaji wa Radio Planet FM ya mjini hapa.

 

 

Baada ya kufanyika maulid hiyo iliyoambatana na kufuturisha iliyofanyika nyumbani kwa Warda maeneo ya Kiwanja cha Ndege Mtaa wa Mtoto wa Boksi, Dida alimuomba Shehe Masenga kumsomea dua hiyo ya kumuondolea mikosi kwenye maisha yake, jambo ambalo shehe huyo alilitekeleza. Baada ya dua hiyo, Wikienda lilizungumza na Shehe Masenga juu ya tukio hilo ambapo alisema: “Hii ni Dua la Husda kwa ajili ya kuondoa mikosi na wasiwasi katika maisha.

“Hivyo huyu dada (Dida) aliniomba nimfanyie dua ambayo kwa hakika, kama ana imani dua yake hiyo itakuwa imepokelewa na Mwenyezi Mungu na maisha yake yatakuwa safi kabisa,” alisema Alhaj Masenga.

 

 

Kwa upande wake, Dida alipotakiwa kuelezea dua hiyo alisema:

“Katika maisha yangu nimekuwa nikiandamwa sana na mikosi, hebu fi kiria, wakati ninatoka Dar kuja hapa (Morogoro), nilipofi ka Maseyu nikiwa peke yangu kwenye gari, nimenusurika kifo baada ya kutaka kugongana uso kwa uso na lori.

 

“Nimeamua kumuangukia Mungu na kumuomba Shehe Masenga anifanyie maombi yatakayoondoa mikosi hii,” alisema Dida akilengwalengwa na machozi.

 

STORI: DUSTAN SHEKIDELE, MOROGORO

Leave A Reply