The House of Favourite Newspapers

Dina: Sanaa hailipi, nimepangiwa nyumba na mtu wangu!

0

dinaNasra Mohamed ‘Dina’

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa Mpaka Home. Kama kawa, kama dawa tunazidi kusonga mbele kila wiki ndani ya safu hii tunakuletea staa ambaye anaanika maisha yake halisi ya nyumbani.

Leo tunaye msanii wa kitambo kwenye anga la sanaa ambaye ameshiriki katika michezo mbalimbali na filamu huyu si mwingine ni Nasra Mohamed ‘Dina’ anayeishi Mwananyamala jijini Dar.
Mwigizaji huyo anasema japokuwa nyumba yake siyo kubwa lakini anaithamini.

Mpaka Home: Vipi mambo, hapa unaishi na nani?
Dina: Nipo mimi na mwanangu.

Mpaka Home: Kazi gani kubwa unayopenda kufanya unapokuwa nyumbani?
Dina: Napenda sana kupika halafu usafi wa nyumba yangu yaani nyumba yangu siyo kubwa lakini naithamini sana.

Mpaka Home: Unaishi mahali pazuri ni kwa ajili ya kazi yako ya sanaa tu au kuna mtu anakupa jeuri?
Dina: Sanaa hailipi sana. Nina mtu wangu ambaye haishi hapa ndiye anayenipa jeuri ya kulipa kodi na mambo mengine.

Mpaka Home: Mara nyingi mastaa hawapendi kuingia jikoni kupika chakula, kwako wewe inakuwaje?
Dina: Mimi bwana naamini kabisa mwanamke bora lazima aingie jikoni mambo ya ustaa naweka pembeni kabisa, huwa napika mwenyewe ndiyo maana unaona hakuna hata dada wa kazi.

Mpaka Home: Kitu gani kinakufurahisha unapokuwa nyumbani?
Dina: Napenda kuangalia tamthiliya mbalimbali zinazonifanya nisitoke ndani kabisa kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Mpaka Home: Nakushukuru sana kwa ushirikiano wako!
Dina: Karibu sana.

Leave A Reply