The House of Favourite Newspapers

Rapa DMX Apata Mtoto wa 15

0

dmx-hhh DMX (1)DMX akiwa na mpenzi wake, Desiree Lindstrom.

DMX (2)DMX aliwahi kuhojiwa mwezi Juni na kusema amezaa watoto na wanawake 9 ambapo kwa sasa wamefika 10

DMX (3)DMX aliwahi kupelekwa mahakamani kwa kushindwa kulipa pesa za matunzo ya watoto kiasi cha dola 400,000.

RAPA maarufu wa ngoma ya Get At Me Dog, Dark Man X ‘DMX’ mwenye umri wa miaka 45 amepata mtoto wa 15 na wa kiume Ijumaa iliyopita (Agosti0 19) kupitia kwa mpenzi wake wa siku nyingi, Desiree Lindstrom.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida la TMZ, mtoto huyo ambaye ni wa kwanza kwa mwanadada  Desiree na wa 15 kwa DMX alizaliwa akiwa na uzito wa Kilogram 2.9 na amempa jina la Exodus Simmons.

1390344749_dmx_kids23_46Inasemekana kuwa wakati mpenzi wake huyo akijifungua, ‘DMX’ hakuwepo hospitalini hivyo alilazimika kupanda kwenye ndege kutoka Arizona hadi New York ili kumuona mwanaye Exodus usiku wa siku hiyo.

Mwaka 2010, DMX alikorofishana na aliyekuwa mkewe Tashera Simmons hivyo kulazimika kuachana akiwa ameishi naye kwa muda wa miaka 11.

trinidad-dmxMpenzi wake mwingine ambaye ni mkazi wa Maryland, Monique Wayne alimzalia DMX mtoto mnamo 2004, huku akidai kuwa rapa huyo alimbaka na kumsababiushia ujauzito huo,hivyo mwaka 2008 kulazimika kumlipa mwanamke huyo pesa kiasi cha dola milioni 1.5.

Mwaka 2013, alitangaza mahakamani kuwa amefirisikajambo ambalo lilitafsriwa kuwa ni moja ya njama zake za kukwepa kuwahudumia watoto wake. Mwaka 2015, alihukumiwa kwenda jela miezi 6 kwa kushindwa kulipa pesa kiasi cha dola $400,000 kwa ajili ya matunzo ya mwanaye.

Leave A Reply