The House of Favourite Newspapers

DODOMA: Ofisa Elimu Hatiani kwa Kuiba, Kusambaza Mitihani WhatsApp – Video

UONGOZI wa Idara ya Elimu ya Halmashauri ya Chemba mkoani Dodoma kwa kushirikiana na waratibu na walimu wakuu wa shule, wameingia kwenye tuhuma nzito ya kupanga kwa makusudi kufanya udanganyifu wa mtihani wa darasa la saba uliofanyika Septemba mwa huu nchini baada ya kudaiwa kuunda makundi ya mtandao wa WhastApp, kuiba mtihani huo na kuusambaza kwenye makundi hayo kwa nia ya kuwasaidia wanafunzi wao.

 

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), Dkt. Charles Msonde,  alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya jinsi mtihani huo ulivyofanyika na kuongeza kuwa tayari wameshawachukulia hatua ikiwemo kutengua uteuzi wao na wengine kuwasimamisha kazi.

 

“Siku moja kabla ya kufanyika, mtihani huo (wa darasa la 7) ulipofika kwenye halmashauri yao waliufungua wakausambazwa kwenye makundi yao ya WhatsApp kwa ajili ya kukokotolewa na kuwafikishia watahiniwa ili kuongeza ufaulu katika shule zao. Uongozi wa Idara ya Elimu Chemba, ulikuwa ukitoa maelekezo namna ya kutimiza lengo hilo la udanganyifu.

 

“Viongozi waliohusika kuvujisha mtihani kwa njia ya WhatsApp, huko Chemba ni Kaimu Ofisa Elimu Msingi, Modest Tarimo; Ofisa Taaluma, Eliakida; Kiongozi wa Kundi la WhatsApp aliyekuwa Mratibu Elimu wa Kata Farukwa, Deo Philip; wakuu wa shule waliokamatwa na waratibu,” alisema Msonde.

 

Aidha, NECTA imeyafuta matokeo ya mtihani wa taifa wa darasa la saba kwa shule zote za msingi za halmashauri ya Chemba na kutangaza kurudiwa tena Oktoba 8 na 9 mwaka huu huku ikitaka mamlaka za ajira kwa mujibu wa sheria za utumishi, kuwachukulia hatua watumishi wote waliobainika kuhusika na udanganyifu huo.

VIDEO: MSIKIE MSONDE AKIZUNGUMZA HAPA

Comments are closed.