Drake Achora Tattoo Kama ya Rihanna
UPDATE: Drake ameamua kuchora tattoo ya samaki papa kwenye mkono wake wa kulia inayofanana na ya mpenzi wake mpya, Rihanna.
Rihanna na Drake wameamua kuanika uhusiano wao ambao umekuwa siri kwa muda wa miezi kadhaa.
Baadhi ya wanahabari na mashabiki za mastaa hao wameeleza kuwa, tattoo hiyo inaashiria jambo flani kati yao ambalo bado hakijajulikana.
Wawili hao wamekuwa gumzo kwa sasa kwenye vyombo vy habari na mitandao ya kijamiitangu walivyoanika uhusiano wao kwenye tuzo za usiku wa Jumapili ya tuzo za VMA.