The House of Favourite Newspapers

Drake Atakomba Tuzo 18 BET?

0

TANGU alipodondosha mixtape yake ya So Far Gone, Drake amekuwa msanii mwenye uhakika wa ‘namba’ kwenye chati mbalimbali za muziki na tuzo.

Kupitia tuzo za mwaka huu, Drake anadhirisha ‘ukubwa’ wake kwenye muziki tangu aliposhika hatamu rasmi muziki mwaka 2009.

Ukizungumzia nominations tatu za mwaka huu kwenye tuzo za BET, usisahau Drake tayari anazo kibondoni tuzo 15 za BET mbali na kuwa na jumla ya nominated 65 katika vipengele tofauti vya tuzo hizo.


Tuzo zake za kwanza alipata mwaka 2010 kama Msanii Bora wa Kiume na Kundi Bora akiwa na Young Money.

Mwaka huu, Drake anawania Msanii Bora wa Kiume wa Hip Hop kwa mara nyingine, Kolabo Bora na Video Bora kupitia nyimbo zake kali alizoshirikiana na DJ Khaled (Popstar) na Lil Durk (Laugh Now Cry Later).

Ni suala la kusubiri na kuona pale Juni 27 mwaka huu washindi watakapotangazwa kama mbabe huyu atazitia kibindoni tuzo hizo zote au la. Endapo akifanikiwa kuzichukua, atakuwa na jumla ya tuzo 18 za BET.


Kwenye Tuzo hizo za BET, kwa mara ya tatu Mbongo Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ naye amekuwa nominated na mara mbili zilizopita, hakufanikiwa kuchukua.

Safari hii, amekuwa nominated kwenye Kipengele cha International Act hivyo naye tusubiri na kuona endapo ataibuka kidedea kwa mara ya kwanza au la.

Credit:

@hotpot_tz

@erick.evarist

 

Leave A Reply