The House of Favourite Newspapers

Drake na Kanye Kizazi Sana

0

MARAPA wa kiwango cha Dunia, Drake na Kanye West; wote wa Marekani, sasa uhusiano wao ni kizazi sana baada ya kumaliza bifu lao la muda mrefu.

Sasa jamaa hao wameungana tena ambapo Kanye ameposti picha akiwa na Drake nyumbani kwake huku Kitaa cha Toronto nchini Marekani.

Za ndani kabisa zinasema kuwa, wamemaliza tofauti zao baada Kanye kutamani wapatane kwa muda mrefu.

Drake na Kanye waliingia kwenye bifu kubwa baada ya Kanye ku-tweet karibia Twitter 25 akim-dis na kumponda Drake kwa kile ambacho Drake wala yeye Kanye hakuwahi kufunguka sababu ilikuwa ni nini.

Hata hivyo, za ndani kabisa zinasema sababu ni Drake kutoka kimapenzi na aliyekuwa mke wa Kanye, Kim Kardashian.

Leave A Reply