The House of Favourite Newspapers

Droo Kubwa… Shinda Nyumba Hii Septemba 27

0
Nyumba mpya ya Global Publishers iliyojengwa katika eneo la Bunju B inayoshindaniwa.

 

BAADA ya wasomaji kukata kuponi zao kwa ajili ya kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili kwa zaidi ya miezi sita, nyumba hiyo ambayo itatolewa kwa mshindi wake, imewekwa hadharani.

Nyumba hiyo ya kisasa imejengwa katika eneo la Bunju B nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na droo kubwa sasa imetangazwa rasmi kuwa itachezeshwa Septemba 27, mwaka huu.

Meneja Mkuu wa Global Publishers, ambao ndiyo waendeshaji wa zoezi hilo kubwa kabisa nchini, Abdallah Mrisho alisema jana kuwa, maandalizi yote kwa ajili ya hafla hiyo ya aina yake yamekamilika na kinachosubiriwa ni siku yenyewe ya tukio, ambayo itakuwa ni Jumatano.

Nyumba mpya ya Global Publishers iliyojengwa katika eneo la Bunju B inayoshindaniwa.

“Tumekamilisha kila kitu, kilichobakia sasa ni kuwaomba wasomaji wa magazeti yetu ya Ijumaa Wikienda, Amani, Uwazi, Risasi, Championi na Ijumaa kukata kuponi zao za mwishomwisho na kuzituma kwetu haraka iwezekanavyo. Kwa wale wa mikoani, kuponi zao wazipeleke kwa wakala wetu ambao wako kila sehemu nchini.

“Kwa wale wa Dar wazilete kuponi zao katika ofisi zetu zilizopo Bamaga, Mwenge na wazikabidhi kwa watu maalum wanaozipokea. Huu ni wakati wa kuhakikisha hawakosi nakala zao kwa vile muda umeshaisha. Wiki mbili zilizobaki wahakikishe hakuna

 mtu anayeziacha kuponi zake bila kuzileta kwetu, kwa sababu huenda ile utakayoiacha nyumbani, ndiyo iliyokuwa ya mshindi,” alisema Mrisho.

Nyumba hiyo ya kisasa imejengwa Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ikiwa na thamani ya mamilioni ya shilingi na itakuwa ni ya pili kutolewa na Global Publishers, kwani katika bahati nasibu ya kwanza iliyofanyika mwaka jana, mjengo kama huo ulitolewa.

Aliyeshinda katika bahati nasibu hiyo ya kwanza alikuwa ni mwanamama mjasiriamali, Nelly Mwangosi mwenyeji wa Iringa ambaye mjengo wake ulijengwa eneo la Salasala, pia nje ya jiji.

Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili inafanyika baada ya kuwepo kwa droo ndogo tano zilizochezeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ambako zaidi ya wasomaji 30 wa magazeti ya Championi, Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikienda waliibuka na zawadi za aina mbalimbali zikiwemo pikipiki, televisheni kubwa, simu za kisasa za mikononi, dinner set na ving’amuzi.

NA MWANDISHI WETU | IJUMAA WIKIENDA

Leave A Reply