The House of Favourite Newspapers

DROO KUBWA SHINDA NYUMBA MAKAZI MAPYA YA MSHINDI YAJULIKANA

0

WAKATI siku ya kuchezesha droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili ikizidi kukaribia, imebainika kuwa mjengo ambao mshindi atapata, umejengwa maeneo ya Bunju B, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

SHINDA NYUMBA YATIKISA TEMEKE

Msomaji wa Vetenari akijaza kuponi.

Ofisa Masoko wa Global Publishers, ambayo ndiyo inayoendesha bahati nasibu hiyo, Keffa Masanga, alisema jana kuwa, nyumba hiyo ya kisasa imejengwa eneo hilo, njia inayoelekea Mabwepande.

“Ni bonge la mjengo kwa kweli, mtu atakayebahatika ku­upata, atakuwa amepata kitu kikubwa sana katika maisha yake,” alisema ofisa huyo.SHINDA NYUMBA YATIKISA TEMEKE

Msomaji akikata kuponi ya Shinda Nyumba.

Naye Meneja Mkuu wa Glo­bal Publishers, Abdallah Mrisho aliwataka wasomaji wa maga­zeti ya Championi, Ijumaa, Iju­maa Wikienda, Risasi, Amani na Uwazi kupeleka kuponi walizok­wishakata kwa mawakala wa magazeti walio kila pembe ya nchi, sambamba na kuzipeleka katika ofisi zao zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

“Ninachoweza kuwaambia wasomaji wa magazeti yetu ni kuwa tumeshamaliza vikwazo vilivyokuwa vinatukabili, droo yetu kubwa itachezwa mwezi huu katika siku ambayo tuta­waeleza hapo baadaye kidogo, tuendelee kufuatilia katika kurasa za magazeti yetu tutajua lini hii shughuli itafanyika,” al­isema Mrisho.

Mrisho aliwataka wasomaji kuendelea kukata kuponi katika magazeti, zinazopatikana katika kurasa za ndani za kila Gazeti la Global Publishers ambayo huuzwa kwa shilingi 500 tu am­bayo ni Championi, Ijumaa Wik­ienda, Risasi, Amani na Uwazi na lile la Ijumaa ambalo huuzwa kwa shilingi 1,000, lakini likiwa na kuponi mbili.

SHINDA NYUMBA YATIKISA TEMEKE

Wasomaji wa Sokota Temeke wakijaza kuponi.

Bahati Nasibu ya Shinda Ny­umba Awamu ya Pili inafanyika baada ya kuwepo kwa droo ndo­go tano zilizochezeshwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ambako zaidi ya waso­maji 30 wa magazeti ya Cham­pioni, Ijumaa, Risasi, Uwazi, Am­ani na Ijumaa Wikienda waliibuka na zawadi za aina mbalim­bali zikiwemo pikipiki, tel­e v i s h e n i kubwa, simu za kisasa za m i k o n o n i , dinner set na ving’amuzi.

Droo hizo ndogo zilifanyika katika maeneo ya Dar Live Mbagala, Manzese Bakhresa, CCM Mwin­juma Mwananyamala na Ma­bibo Soko la Ndizi, matukio am­bayo yalihudhuriwa na mamia ya wasomaji.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa kampuni hiyo kucheze­sha bahati nasibu na kutoa zawadi ya ny­umba baada ya mwaka jana kufan­ya hivyo ambapo mjasiriamali kuto­ka Iringa, Nelly Mwangosi aliji­patia zawadi hiyo kubwa ambayo imebadili maisha yake ambayo sasa yamekuwa bora zaidi.

Bahati Nasibu hiyo ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Premier Bet.

Leave A Reply