The House of Favourite Newspapers

DSTV Yaja na ‘Kitu Juu Kitu Kitu’ Ili Umwone Samatta EPL

0

Msanii maarufu wa filamu nchini Jacqueline Wolper (kushoto), akifuatiwa na mkongwe wa Bongo Fleva, Dully Sykes, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo,  na Mkuu wa Kitengo cha Thamani kwa Wateja, Hilda Nakajumo wakati wa uzinduzi wa kampeni maalum ya DSTV ya ‘Tia Kitu Pata Kitu’ iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuwashangaza wateja wake kwa punguzo kubwa la bei ya vifurushi vya DStv, Kampuni ya MultiChoice Tanzania leo Januari 21, 2020,  imefungua mwaka kwa ofa ya aina yake, ambapo sasa mteja akilipia kifurushi chake huzawadiwa kifurushi cha juu yake bila malipo ya ziada.  

Ofa hii ambayo imepewa jina la ‘Kitu juu ya Kitu’ imeanza rasmi ambapo sasa mteja wa DStv akilipia kifurushi chake atapatiwa kifurushi cha juu yake bila gharama za ziada na hivyo kuweza kupata chaneli za kifurushi cha juu kuliko kile alicholipia.  

Mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja wa MultiChoice Tanzania, Hilda Nakajumo, amesema ofa hiyo ni kwa wateja wote wa DStv kuanzia kifurushi cha Bomba hadi wale wa kifurushi cha Compact Plus.

“Ofa hii ni mahsusi kwa wateja wetu wa kuanzia kifurushi cha Bomba hadi Compact plus na kila mteja atakayelipia kifurushi chake atapandishwa daraja kwenda kifurushi cha juu yake ndani ya muda wa saa 48” alisema Hilda.  

Akielezea zaidi kuhusu ofa hiyo amesema kwa mfano mteja wa kifurushi cha Bomba cha Sh 19,000 akilipia kifurushi chake, moja kwa moja atapandishwa daraja na kupelekwa kifurushi cha Family cha Sh. 29,000 bila kulipia gharama za ziada.  

Amefafanua kwamba wakati wote MultiChoice Tanzania imekuwa kinara katika kuwapatia wateja wake wa DStv burudani kabambe kwa gharama nafuu na ndiyo sababu mwishoni mwa mwaka jana walishusha bei za vifurushi vyao kwa hadi asilimia 36.  

“Suala la kuwapatia wateja wetu huduma bora na kwa gharama nafuu ni la msingi sana katika mipango na mikakati yetu. Tunataka Watanzania wasipungukiwe na burudani kuanzia michezo, tamthilia, maigizo, filamu mbalimbali, makala, habari na vipindi mbalimbali.

“Kwa ofa hii kabambe, tunaamini wateja wetu watakuwa na kila sababu ya kuufurahia mwaka mpya kwani sasa tunawapa kitu juu ya kitu! Ni kiasi tu cha kulipia akaunti yako na kufurahia ofa hii,” alisema.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa MultiChoice Tanzania, Ronald Shelukindo, amesema ofa hii ni ya aina yake huku akitoa mfano kwa wapenda soka ambapo kwa mteja wa kifurushi cha Family cha Tsh 29,000 akilipia atapandishwa hadi kifurushi cha Compact cha Tsh 44,000 na hivyo kushuhudia ligi kubwa duniani ikiwemo michezo yote ya ligi kuu ya Uingereza bila kusahau La liga, Serie A na michuano mingine mikubwa ulimwenguni.  

Akizungumza katika hafla ya kutangaza rasmi ofa hiyo, msanii mkongwe hapa nchini, Dully Sykes, amesema amefurahi kuona DStv ambayo amesema nayo ni kongwe kama yeye alivyo msanii mkongwe, kuwa inatoa ofa kabambe kwa wateja wake huku akiishukuru kampuni hiyo kwa kuwa na utamaduni wa kuwatumia wasanii wa ndani katika shughuli zake mbalimbali.  

“DStv Tanzania wamekuwa na utamaduni wa kutumia Watanzania katika matangazo yao na shughuli zao mbalimbali, hili ni suala la kujivunia sana na mimi binafsi najivunia kufanya kazi na DStv kwani ni brand kongwe kama mimi mwenyewe nilivyo brand kongwe” alisema Dully Sykes.  

Ofa hii maalumu inaendeshwa kwa kufuata vigezo na masharti na inategemewa kuendelea hadi mwisho wa mwezi Februari na inawahusu wateja wote wanaolipia vifurushi walivyo sasa na hivyo kupandiswha kifurushi cha juu zaidi.  

Wateja wa DStv Premium hawahusiki na ofa hii kwani tayari wapo kwenye kifurushi cha juu kabisa na pia wananufaika na ofa nyingine ya ‘DStv Thanks’ inayowawezesha kupata punguzo kubwa la bei kwenye maeneo mbalimbali kama vile Serena Hotel, Nakiete Pharmacy Mikocheni, S. H. Amon,  mgahawa wa Spurs Masaki na maeneo mengine mengi kote nchini.  

Wateja wengine ambao hawawezi kunufaika na ofa hii ni wale wa VIP, wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania, akaunti za biashara, akaunti zilizolipiwa kwa miezi mitatu na akaunti za mwaka.

 

Leave A Reply