The House of Favourite Newspapers

Dube Aikataa Tuzo ya Kagere Bara

0

KINARA wa chati ya ufungaji Bongo, Mzimbabwe Prince Dube ameibuka na kubainisha kwamba akili yake ni kuendelea kufunga mabao ambayo yataifanya klabu yake kuwa mabingwa wa ligi na siyo kutwaa kiatu cha ufungaji bora.

 

Dube ameongeza kwamba akili yake ni kuendelea kufunga mabao kwa ajili ya timu yake huku suala la kuwa mfungaji bora akiliweka mwishoni mwa msimu.

 

Mzimbabwe huyo kwa sasa ndiye kinara wa ufungaji Bara akiwa na mabao matano akifuatiwa na Mnyarwanda Meddie Kagere mwenye mabao manne.

Dube ameliambia Championi Jumatano, kuwa kwa sasa hana mawazo na kuwa mfungaji bora kwa sababu ya kujitolea kwa ajili ya timu yake kufikia malengo yao ya kuwa mabingwa.

 

“Kuhusu suala la kuwa mfungaji bora kwa wakati huu hapana kwa sababu nafanya majukumu kwa ajili ya timu.

 

“Mabao ninayoyafunga nataka yaisaidie timu kufikisha malengo yake ya kuwa mabingwa tofauti na mimi kuwa mfungaji bora na kama ikiwa hivyo basi iwe mwishoni mwa msimu,” aliweka nukta Dube.

 

Msimu uliopita Kagere alichukua tuzo hiyo kwa kufanikiwa kufunga mabao 22.

Stori: Said Ally, Dar es Salaam

Leave A Reply