The House of Favourite Newspapers

RC Kigoma Awajulia Hali Zitto, Wenzake Waliopata Ajali

0

MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, amemtembelea na kumpa pole  Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma baada ya kupata ajali ya gari juzi wakati akiwa katika shughuli zake za kampeni.

 

Amepata ajali katika kata ya Kalya baada ya gari alilokuwa amepanda kugongwa na gari lingine kwa nyuma na kusababisha majeruhi kwa watu waliokuwa katika gari hilo ambapo huduma ya kwanza walipatiwa katika Kituo cha Afya Kalya.

Zitto amesema gari lililowagonga na kusababisha ajali yao ni la mgombea ubunge Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi  ya ACT  Wazalendo, chanzo kikiwa ni vumbi lililokuwa limetanda barabarani, ambapo amesema hali yake inaendelea kuimarika.

 

“Kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa afya nimeambiwa kuwa bega langu la mkono wa kushoto lina tatizo ambapo kuna mfupa ambao umevunjika, lakini naendelea vizuri kwa sasa,” amesema Zitto.

 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dkt. Simon Chacha, ameeleza kuwa huduma zinaendelea kutolewa kwa majeruhi wote na kuwa Zitto alitarijiwa kusafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu  na vipimo zaidi.

Leave A Reply