Kartra

Dube Aongeza Mkataba wa Miaka Miwili Azam FC

NYOTA wa Klabu ya Azam FC, Prince Dube ameongeza mkataba wake ndani ya kikosi hicho kwa muda wa miaka miwili.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Azam FC imeeleza kuwa nyota huyo atasalia ndani ya timu hiyo mpaka 2024.

Nyota huyo ni namba moja kwanutupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ametupia mabao 14 na ana pasi tano za mabao.

Pia ana mabao matatu katika Kombe la Shirikisho ambapo Azam FC imetinga hatua ya nusu fainali na itacheza na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

 


Toa comment