The House of Favourite Newspapers

Dude: Kifo cha Dogo Mfaume kitufunze

0
Kulwa Kikumba ‘Dude’.

STORI: MWANDISHI WETU, RISASI JUMAMOSI, MOTOMOTO NEWS

SIKU chache baada ya kufariki dunia kwa mkali wa Muziki wa Mchiriku na Mnanda, Dogo Mfaume, nyota wa filamu nchini, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amewataka watu maarufu ambao ni kioo cha jamii, kujitambua na kuwa mfano bora kwa kufanya mambo mazuri.

Aliyekuwa mkali wa Muziki wa Mchiriku na Mnanda, Dogo Mfaume.

Akizungumza na Za Motomoto News, Dude aliyeshiriki katika fi lamu iitwayo Why, ambayo sehemu kubwa imechezwa ndani ya ndege ikiwa angani, alisema mastaa wanapofanya jambo baya, kama utumiaji wa madawa ya kulevya, huwafanya mashabiki wao vijana, kuamini kuwa kinachofanywa ni kitu kizuri hivyo hujaribu kuiga.

“Nimesikitishwa sana na kifo cha Dogo Mfaume kwa sababu aliutoa Mnanda mtaani na kuuleta ukumbini, wakati wake alipata mashabiki wengi hasa vijana, sijui ni wangapi walimfuata katika utumiaji wa unga, lakini nadhani angekuwa anafanya vitu vizuri angekuwa balozi mzuri sana. Nitoe rai kwa mastaa, tujitahidi kuwa mabalozi wazuri kwa manufaa ya jamii yetu,” alisema Dude

Leave A Reply