The House of Favourite Newspapers

Dullvan Ana Vijora Zaidi Ya 50

0

KIJANA mdogo ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kupitia kuchekesha kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Instagram, Abdallah Sultan ‘Dullvan’ amesema kuwa, anaweza kuwa na vijora vingi kushinda hata baadhi ya wanawake.

 

 

Anasema kuwa, kila mara ananunua vijora kwa ajili ya kuigizia. Katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Dullvan anasema kuwa, mara nyingi anapenda dukani ni kwa ajili ya kununua vijora kuliko hata nguo za kawaida, jambo ambalo hata yeye kuna wakati anajishangaa.

 

Anasema kuwa, watu wanaweza kushangaa, lakini ukweli unabaki kuwa anaipenda kazi yake ya kuchekesha ndiyo maana anafanya yote hayo na wala hajali kabisa. “Huwezi kuamini, ukweli ni kwamba nina zaidi ya vijora 50, kazi yangu ni kubadilisha rangi tu.

 

Hiyo yote ni kwa sababu ninaipenda kazi yangu na ninaoneshea uhalisia; yaani hata nguo zangu za kawaida siyo nyingi kama ilivyokuwa kwa madera; yaani kuna wakati hata mimi ninacheka mwenyewe na hata wauza vijora ikitoka dizani mpya, wananiita,” anasema Dullvan ambaye hivi sasa anatamba na vichekesho kwenye Kipindi cha Kitimtim.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply