The House of Favourite Newspapers

EFM Wazindua Jogging Club

0

EFM (1) EFM (2) EFM (3) EFM (4) EFM (5) EFM (6)

DCIM100MEDIADJI_0073.JPG
Vikundi zaidi ya 30 vya Jogging kutoka sehemu mbalimbali za jiji wakiendelea.

KITUO cha radio cha EFM kinachorusha matangazo yake kutokea Kawe jijini Dar es Salaam, kimezindua Jogging Club ikiwa ni  kwa ajili ya mazoezi ya kujenga mwili na kuimarisha afya za washiriki.

Uzinduzi huo umefanyika jana katika viwanja vya Tanganyika Packers, vilivyopo Kawa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na vikundi zaidi ya 30 vya Jogging kutoka sehemu mbalimbali za jiji.

Aizungumza kwenye hafla hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemiah Mchechu,  amekipongeza kituo hicho kwa kuanzisha kikundi hicho akisema ni ishara nzuri ya kuimarisha afya za wananchi watakaoshiriki.

“Nawapongeza sana EfM kwa kuanzisha kikundi cha jogging kwani ni jambo zuri na pia nawaomba wananchi na wasikilizaji wa radio yenu kuitikia wito wa kufanya mazoezi kwani mazoezi ni afya,” alisema Msechu.

 

Uzinduzi huo ulianzia ofisi za radio hiyo Kawe ambapo washfiriki walikwenda hadi Mwenge na kuishia viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, ambapo ulikwenda sambamba na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii kadhaa wakiwemo Man Fongo na Sholo Mwamba.

(Picha/ Habari: Hilaly Daudi/GPL)

 

Leave A Reply