The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli aongoza Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa

0

 OTH_9375

Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi baada ya kuweka silaha za jadi katika Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa alipoongoza Madhimisho ya Siku ya Mashujaa mjini Dodoma leo Julai 25, 2016. m24 IMGS7857Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa  mjini Dodoma , Julai 25, 2016. Watatu kulia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi , Jenerali Davis Mwamunyange na kulia ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu.

IMGS7855Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Inspekta Jenerali wa Polisi, Ernest Mangu, Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Davis Mwamunyange na Kamishina Jenerali wa Magereza John Minja(kulia)m katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa  mjini Dodoma , Julai 25, 2016. IMGS7851Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali , Davis Mwamunyange katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. 

IMGS7837Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Meya wa manispaa ya Dodoma, Jafari Mwanyembwa  katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016.

IMGS7817Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda  katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula  na watatu kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu ,John Malecela.

IMGS7797Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma , Julai 25, 2016. 

IMGS7785Wananchi wa Dodoma waliojitokeza kushiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Dodoma wakimsikilza Rais John Maguguli wakati alipozungumza kwenye maadhimisho hayo mjini julai 25, 2016.

IMGS7771Rais John Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi,Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.  Kulia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubei Ali Maulid na wapili kulia ni Spika wa Bunge, Dkt, Tulia Ackson.

IMGS7766 Rais John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein katika Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kwenye uwanja wa Mashujaa, Julai 25, 2016.46954b28-c154-4f01-bfd4-6da1969940e2.jpem16

IMG_0395Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli akiweka Mkuki na Ngao katika kilele cha maadhimisho ya siku ya mashujaa katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma leo IMG_0344Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Samia Sulihu Hassan mara alipowasili katika Maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Mnara wa Mashujaa Mjini Dodoma leo. IMG_0313Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi mara  alipowasili katika Maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Mnara wa Mashujaa Mjini Dodoma leo IMG_0287Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali alipowasili katika Maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Mnara wa Mashujaa Mjini Dodoma leo. DSC02368Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe, Dkt.John Pombe Magufuli akipokea heshama ya gwaride la Vikosi vya Ulinzi katika maadhimisho ya kilele cha siku ya mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa mashujaa Mjini Dodoma leo. DSC02362 DSC02357 OTH_9308Shughuli za maadhimisho hayo ya siku ya Mashujaa zilipokuwa zikiendelea ndani ya uwanja huo wa Mashujaa. m28 Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Malecela baada ya kuongea na wananchi kwenye Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.

OTH_9425Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016 m27Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein akiongea wakati wa Madhimisho ya Siku ya Mashuja mjini Dodoma leo Julai 25, 2016.

PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuwaenzi Mashujaa kwa kudumisha Amani, Umoja na Utulivu uliojengwa na mashujaa hao. Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo tarehe 25 Julai, 2016 wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa, yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa Mjini Dodoma.

Pamoja na kutoa rai hiyo Rais Magufuli ameahidi kuwa atahakikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma inatekelezwa kabla ya kuisha kwa kipindi chake cha uongozi wa miaka mitano.

“Tunapoadhimisha siku ya Mashujaa hatuwezi kumsahau Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Baba wa Taifa alisema makao makuu yawe Dodoma, haiwezekani sisi watoto wake, sisi wajukuu wake tupinge kauli ya Mzee huyu.

“Kwa hiyo nilikwishazungumza na leo narudia hili katika siku ya Mashujaa, mlinichagua ndugu zangu wa Dodoma kwa kipindi cha miaka mitano, hadi sasa miezi minane imepita, nimebakiza miaka minne na miezi minne, nataka kuwathibitishia kuwa katika kipindi cha miaka minne na miezi minne iliyobaki nitahakikisha serikali yangu pamoja na mimi tunahamia Dodoma bila kukosa” Amesema Rais Magufuli.

Kufuatia maelekezo hayo ya Mhe. Rais, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameagiza Mawaziri wote waanze mara moja kuhamia Dodoma na kwamba yeye mwenyewe atakuwa amehamia Dodoma ifikapo mwezi Septemba mwaka huu.

Viongozi wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid, Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe. John Samwel Malecela na Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mabalozi na wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa vyama vya siasa na dini, maafisa na askari waliopigana vita mbalimbali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma

Leave A Reply