The House of Favourite Newspapers

Erasto Nyoni, Kichuya wana vituko Stars

MASTAA wa Taifa Stars, Shiza Kichuya na Erasto Nyoni wana vituko mazoezini ambavyo vinachangia kuongeza morali kwa wenzao. Katika mazoezi ya juzi yaliyofanyika Uwanja wa Boko yaliyoshuhudiwa na Spoti Xtra linaloongoza kwa kusomwa Alhamisi na Jumapili, Nyoni na Kichuya walikuwa kivutio cha kipekee.

 

Mara baada ya kufika Uwanja wa mazoezi wa Boko nje kidogo ya mji, Nyoni alishuka kisha akamsubiri bosi wake (pale Simba) John Bocco na kuanza kumsukuma ili awahi mazoezini huku akimtania na wote wakawa wanacheka kabla ya kumfuata Mudhathir Yahya, Hasan Kessy na Himid Mao ambao wote aliwaacha wakivunjika mbavu baada ya kuwaambia jambo fulani.

 

Kichuya ndio balaa, yeye baada ya kushuka kwenye gari kituo cha kwanza kwenye mipira ambapo alikaa juu ya mpira na kuanza kuwapigisha stori wachezaji wenzake ambao nao aliwaacha hoi.

 

Kituko kingine alifanya baada ya kumaliza kusali wachezaji wote wakiwa wameshikana mikono na kuunda duara yeye akaingia katikati na kuanza kuwatazama kama kwamba anataka kuwatangazia kitu fulani wote wakagundua alikuwa anawazingua wakabaki kucheka.

LUNYAMADZO MLYUKA

Comments are closed.