The House of Favourite Newspapers

Esha Buheti: Ukweli Ndiyo Unaoniponza

0

Msanii wa filamu nchini, esha buheti ameeleza kuwa tabia yake ya kusema ukweli ndiyo inayomponza mpaka wasanii wenzake wanamuona mnafiki wakati siyo kweli.

 

Akizungumza na amani, esha alisema siku zote watu huwa hawapendi kuambiwa ukweli bali wanataka kusifiwa hata kama wamefanya vitu vibaya, jambo ambalo kwake halina nafasi. Hivyo akiona mtu anastahili pongezi atampongeza na kama hastahili basi atampa makavu, haijalishi atalichukuliaje.

 

“sipendi mambo ya unafiki kabisa, yaani kama ni nyeusi nitakuambia nyeusi na kama ni nyeupe nitakuambia nyeupe. Siwezi kukusifia wakati naona unapotea, nitasema ukweli ili ujirekebishe, hivyo ndivyo nilivyolelewa hata kama wananiona mnafiki na sifai, hilo halinipi shida na siwezi kubadilika,” alisema esha.

Stori: Memorise Richard.

Leave A Reply