The House of Favourite Newspapers

Esha Buhet: Mimba Imeongeza Mahabati Kwa Mume

1
Staa wa filamu Bongo, Esha Buhet akiwa na mumewe aitwaye Nico.
Nico akiwa ameshia tumbo la mkewe.
Esha akiwa kajiachia sebureni kwake.
Akisoma meseji za marafiki zake katika mitandao ya kijamii.

Akiandaa madikodiko ya kupika.
Esha akiwa na mtoto wake Clarisa wakiselfika.
Akiwa mbele ya ndiga yake anayotumia katika mishe zake mjini.

IMELDA MTEMA -0713 612533 | RISASI JUMAMOSI |MPAKA HOME

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa safu hii tamu ya Mpaka Home, kazi yangu hapa ni moja tu, kuhakikisha kila wiki namtembelea staa mmoja na kukujuza maisha yake halisi. Wiki hii tunaye staa wa filamu Bongo, Esha Buhet, ambaye ameyaweka wazi maisha yake ya kila siku alipotembelewa na safu hii nyumbani kwake, Kijitonyama-Mabatini jijini Dar ambapo anaishi yeye na mumewe aitwaye Nico na mtoto wao Clarisa. Twende pamoja hapa chini ili uweze kujua mengi zaidi:

MPAKA HOME: Vipi Esha, kwanza mashabiki wako wangependa kupata ratiba yako ya siku nzima ikoje?
ESHA: Siku hizi naamka asubuhi na mapema nafikiri kutokana na hali hii ya ujauzito nilionao, cha kwanza kabisa naingia jikoni kuandaa chai na kupika chapati maana nazipenda sana, baada ya hapo nafanya usafi wa mwili wangu ndipo ratiba nyingine zinaendelea.

MPAKA HOME: Namuona baba yuko bize kukuwekea vitu vyako, anafanya hivyo kila siku au kwa sababu kaniona?
ESHA: Hapana ndiyo maisha yetu tena kwa kipindi hiki cha ujauzito mahaba yamezidi sana mpaka nafurahi.

MPAKA HOME: Watu wengi wakiwa katika hali ya ujauzito hawataki kuingia jikoni wewe ni vipi?

ESHA: Kwangu ni tofauti, mimba yangu inapenda niingie jikoni.

MPAKA HOME: Leo nimemkuta mwanao Clarisa maana mara nyingi sikumkutagi hapa nyumbani anakuwepo wapi?

ESHA: Huyo siku zote anakuwa kwa bibi yake tangu akiwa mdogo kwa kuwa anampenda sana.

MPAKA HOME: Nini unakipenda zaidi kukifanya unapokuwa nyumbani?

ESHA: Mimi ni jikoni wakati wote.

MPAKA HOME: Kuna kipindi ziliibuka tetesi kuwa wewe na mumeo mlitengana unazungumziaje hilo?

ESHA: Hakuna ukweli wowote, kama unavyojua watu wakiona watu wanapendana wanaweka fitina, sisi tupo
vizuri.

MPAKA HOME: Kuna kipindi ulikuwa nchini Nairobi takriban miaka miwili ukifanya kazi, vipi kuhusu mumeo ulimuachaje?

ESHA: Roho ilikuwa inadunda sana lakini kikubwa ni kuaminiana tu, nilikuwa nikimuomba Mungu wakati wote nimkute salama bila kuingiwa na vishawishi.

MPAKA HOME: Unaonekana kujiachia sana na ujauzito wako kama ndiyo mara ya kwanza kupata mtoto ni kwa nini?
ESHA: Yaani huu ujauzito niliutafuta kwa muda mrefu ndiyo maana naufurahia.
MPAKA HOME: Vipi kuhusu kuigiza maana umepotea kwenye filamu kitambo sasa?

ESHA: Nimeamua kupumzika kwanza hadi Mungu akinijalia nikijifungua salama ndipo nitaanza tena.
MPAKA HOME: Nakushukuru Esha kwa ushirikiano wako.
ESHA: Ahsante na karibu tena wakati mwingine.

1 Comment
Leave A Reply