The House of Favourite Newspapers

Exclusive… Uwoya: Msiniige Mtaumia, Hamjui Nimepitia Msoto Gani Mpaka Kufikia Hapa

0
Irene Pancras Uwoya.

Irene Pancras Uwoya; ni mwanamama kinara wa Bongo Movies mwenye mvuto wa kipekee nchini Tanzania ambaye anasema kuwa, huu ni wakati wake wa kufurahia mafanikio huku akiwataadharisha wanamuiga akisema; “Msiniige Mtaumia…”

 

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Uwoya anasema kuwa, huu mwezi ni wake wa kula bata mwanzo hadi mwisho.

 

ZIARA NDANI NA NJE YA NCHI

Uwoya anasema kuwa, hii ni kwa sababu huu ndiyo mwezi wake wa mafanikio makubwa hivyo amejipangia kufurahi kwa kufanya ziara kubwakubwa ndani na nje ya Tanzania.

Uwoya anasema kuwa, ana furaha mno na amepanga kuzunguka sehemu tofauti nchini kwa ajili ya kufurahi kwa sababu ana amani kubwa mno moyoni mwake.

 

KWENDA KUMALIZIA MEXICO

Mama huyo wa mtoto mmoja anasema kuwa, amepanga akimaliza ziara ya hapa Bongo, basi ataenda kumalizia nchini Mexico ambako kuna viwanja vya bata vya kutisha.

 

“Yaani ni mwezi wa mafanikio na baraka tele kwangu, nataka kwanza nizunguke hapa Bongo nikiinjoi na nikiimaliza tu naenda zangu Mexico kwa ajili ya kumalizia raha zangu; yaani ni hivi, ni bandika bandua aisee, lakini waambie wanataka kuiga wataumi,” anasema Uwoya.

CHAWA ARISTOTE APIGILIA MSUMARI

Kwa upande wake, Aristote ni Chawa wa Uwoya ambaye anasema kuwa, kila wanachopenda kumuiga kina madhara yake siku zote hivyo wajifunze au vitu vingine waviangalie tu na kuviacha vipite kama vilivyo.

Aristote nasema kuwa, wapo wengine wanataka kuwa kama alivyo Uwoya ndani ya siku moja, jambo ambalo haliwezekani kwani wakifanya hivyo wataumia.

 

“Wasijaribu kuiga, wataumia, hawajui mtu amepitia msoto gani mpaka kufikia hapo alipofikia.

“Irene (Uwoya) sasa hivi anahitaji maadui wapya, wale wa zamani wameshakuwa marafiki, wawe wavumilivu wa kila kitu maana wasifikiri kila kitu ni rahisi tu, haiwezekani na siyo kila kitu cha kuiga maana mtu atajikuta anaumia bure,” anasema Aristote akisisitiza watu wamuache Uwoya ainjoi maisha yake.

 

Tambo hizo za Uwoya zinakuja siku chache baada ya kuwa mwathirika mwingine wa kusambaa kwa picha na video zake za ngono.

 

Baadhi wafuasi wa Uwoya wanaamini kuwa, pamoja na kuwa na pesa nyingi kiasi cha kuzitapanya kwa starehe za kufuru na kuwamwagia watu, lakini zilishindwa kumnusuru kwenye janga hilo.

 

Watu wa kada mbalimbali wamekuwa na maoni tofauti huku wengi wakijiuliza kwa nini Uwoya alishindwa kuizima ishu hiyo wakati ana pesa za kutosha na kila siku anajitangaza kuwa ni tajiri wa kutupwa.

Wanajiuliza ameshindwaje kuzuia kuchafuka kiasi hicho ilihali taarifa alikuwa nazo mapema kwamba siku yoyote mzigo utavuja?

 

Wiki kadhaa zilizopita Uwoya alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kanisa moja mjini Morogoro lililokuwa likiadhimisha miaka minane tangu kuanza kutoa huduma.

 

Pia Uwoya alikuwa mgeni rasmi wa kuzungumza na kikundi cha kina mama kanisani hapo.

 

Wengi baada ya kuona hivyo waliamini kwamba Uwoya mwisho wa siku ameupokea wokovu na kuacha mambo ya hovyo ila ndiyo tena sasa limempata baya zaidi la kuchafua jina lake kabisa.

Stori; Imelda Mtema, Dar

Leave A Reply