The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Yoweri Museveni Aahidi Kuimarisha Jeshi la Uganda

0

Mtoto wa kiume wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameahidi kupambana na ufisadi ndani ya jeshi baada ya kuchukua usukani kama kamanda wa juu, hatua inayoonekana kwa kiasi kikubwa kuharakisha hatua ya kuelekea kumrithi baba yake.

Museveni mwenye umri wa miaka 79, ambaye ameiongoza Uganda kwa miaka 38 alimtangaza mtoto wake Muhoozi Kainerugaba, mwenye umri wa miaka 49 kuwa mkuu wa jeshi la taifa hilo la Afrika Mashariki wiki iliyopita.

Kwenye hafla rasmi ya kukabidhiwa madaraka Alhamisi, Kainerugaba aliapa ‘kuimarisha ustawi wa wanajeshi kwa kupambana na tatizo la ufisadi pamoja na utawala mbaya wa rasilimali zilizopo,’ kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi.

Jeshi la Uganda linashikilia nafasi muhimu kieneo, wakati likiwa na vikosi vya kulinda amani kwenye mataifa ya Somalia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako vinakabiliana na makundi ya wanamgambo wa kiislamu.

Upinzani nchini Uganda umemshutumu Museveni kwa kumpandisha cheo mwanawe katika jeshi, kwa nia ya kumuandaa kuchukua uongozi wa kisisasa, madai ambayo Museveni amekuwa akikanusha.

ALIYETAKA KUVUNJIWA NYUMBA ARUSHA AKUBALI KUMLIPA MWENZIE MBELE YA WAZIRI SILAA…

Leave A Reply