The House of Favourite Newspapers

Fahamu Ugonjwa wa Zika na dalili zake-2

0

children-born-with-microcephaly
Baada ya wiki iliyopita kueleza ugonjwa huu wa Zika unaambukizwaje na kufafanua dalili zake, leo tutajikita kuelimisha kuhusu tiba na kinga tukiamini kwamba wasomaji watazingatia haya. Endelea:

TIBA

Homa ya Zika inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka. Hakuna dawa maalum ya ugonjwa huu wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana na dalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji na damu.

KINGA

Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au kunyunyizia viuatilifu vya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo, ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile; vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.

ugonjwa.Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu na hakikisha kuwa maua yanayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama, funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara.

Kutumia viuatilifu vya kufukuza mbu yaani mosquito repellants, vaa nguo ndefu ili kujikinga na kuumwa na mbu na tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu pia weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi.

Leave A Reply