The House of Favourite Newspapers

Fahyma Afunguka Kuwa na Stresi

0

MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania ambaye ni baby mama wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’, Faima Msengi au Fahyma amefunguka juu ya tetesi za kuwa na msongo wa mawazo (stresi) akieleza anachokifanya ikimtokea hali kama hiyo.

 

Fahyma anasema kuwa, akiwa na msongo wa mawazo huwa anapenda kulala kukwepa usumbufu utakaomuongezea mawazo. “Nikiwa na stresi napenda sana kulala tu na asinisumbue mtu yeyote mpaka nitakapoamka mwenyewe,” anasema Fahyma.

 

Tangu aachane na Rayvanny, Fahyma anadaiwa kutokuwa kwenye wakati mzuri huku watu wengi wakiamini kuwa huwenda anasumbuliwa na msongo wa mawazo.

Baada ya kuachana na Fahyma, Rayvanny alikwenda kujituliza kwa Paula Kajala ambaye ni mtoto wa mwanamama mwigizaji wa Bongo Movies, Kajala Masanja.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply