The House of Favourite Newspapers

Fahyma Matashtiti Kama Yote

0

BAADA ya kupita kwenye kipindi kigumu cha kuachwa na Rayvanny ambaye sasa anaminya kimapenzi na Paula Kajala, mwanamama Fahyma amejifuta na kurejea kwenye ubora wake akionesha matashtiti kama yote.

 

Baada ya kulamba dili la ubalozi hivi karibuni, sasa hivi ametangaza kwamba hataki dharau baada ya kumjibu kwa ukorofi wakati watu walishamzoea kuwa ni mtu mpole na wala alikuwa hajibu kwa hasira.

 

Fahyma ameposti picha matata kwenye ukurasa wake wa IG ambapo mmoja wa wafuasi wake alimwambia; “Subiri Ray aje akufanyie madharau na mwanamke mwingine coz amekujua wewe huna pa kwenda, siwezi kutamani kuwa na tabia kama yako hata nikaongezwa na pesa juu siwezi kuwa kama wewe, umeshawahi kujua unafanana na mjusi eti unajiita Fahyvanny…”

 

Hapo ndipo Fahyma alipotibuka na kuweka upole pembeni kisha kumjibu; “Jidanganye hivyohivyo my friend, makasiriko ni mengi mno jamani, kuachwa niachwe miye, tabu upate wewe?”

Leave A Reply