The House of Favourite Newspapers

Faiza: Masingo Mama Chuki Zinatuponza

0

MWANAMAMAanayekiwasha kunako Bongo Movies ambaye ni mmoja wa masingo-mama, Faiza Ally amefunguka kuwa, kinachowaponza baby mama wengi waliozaa na wanaume ambao hawaishi nao, ni chuki zisizokuwa na kichwa wala miguu.

 

Faiza huko nyuma alikuwa na mgogoro mzito na baba mtoto wake aitwaye Sasha aliyezaa na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya-Mjini, Joseph Mbilinyi au Sugu, lakini baadaye alijifunza shida ilipokuwa baina yao.Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Faiza anaweza wazi kuwa, chuki zinazoendelezwa na wazazi, moja kwa moja zinawaathiri kwa kiasi kikubwa watoto na kukosa furaha;

 

IJUMAA: Habari Faiza, unaendeleaje?

 

FAIZA: Salama kabisa, Mungu ni mwema, tunaendelea kupambana siku zote.

 

IJUMAA: Vipi kuhusu biashara, inaendeleaje?

 

FAIZA: Biashara ina changamoto kubwa sana kwa sasa, lakini Mungu ni mwema, naendelea vizuri maana tangu Corona ilivyoingia biashara zimeyumba mno.

 

IJUMAA: Kidogo siku hizi naona umetulia sana hata kwenye mitandao tufauti na zamani, kulikoni?

 

FAIZA: Unajua sasa hivi mimi nimejikita zaidi kwenye biashara, inagwa nimekutana na changamoto nyingi sana, lakini ukweli ni kwamba naendelea kupambana.

 

IJUMAA: Nimeona kama sasa hivi Sasha yupo karibu na baba yake tofauti na siku za nyuma na mara nyingi unamsifia…

 

FAIZA: Nilikaa na kujifunza vitu vingi sana, nikagundua kuwa kuna vitu tunakosea kama mabebi mama, hatutakiwi kuonesha tofauti zetu wazi hadi watoto wetu wakaona na wao wakatengeneza chuki hivyo ndiyo maana unaona sasa kila kitu kinakwenda sawa.

 

IJUMAA: Ila Faiza kuna kuna watu huwa wanakutibua kwenye Instagram, una majibu f’lani aisee mpaka najiuliza huwa unayatoa wapi?

FAIZA: (kicheko) unajua kuna watu wanaweza kukurupuka huko na siku wakakukuta una vitu vyako kichwani, halafu wanakuambia kitu ambacho kinakukera, lazima uende naye sawa.

 

IJUMAA: Faiza wewe na Zamaradi mna tofauti yoyote? Maana inaonekana hamko kama mlivyokuwa zamani…

FAIZA: Hapana, tuko vizuri sana, hata juzi watu hawakutuona tunafungua shampeini wote?

 

IJUMAA: Ulisemaga unapenda sana watoto, sasa huna mpango wa kuzaa tena mtoto mwingine?

FAIZA: Natamani kwelikweli, lakini si unaona maisha yalivyo magumu kupita kiasi hivyo tunapambana vilivyo, kwa hiyo ngoja nisubiri kidogo.

IJUMAA: Kuna habari kuwa una mjengo wako wa hatari na umetokana na biashara zako unazofanya, je, ni kweli?

 

FAIZA: Huo mjengo ninao muda mrefu sana, upo nyumbani kwetu Dodoma na tunaendelea kupambana ili mambo yakae sawa.IJUMAA: Kuhusu kuolewa vipi?

FAIZA: Hiyo ishu nimeachana nayo kabisa, napambana tu kila kukicha mambo yaende, hicho ndicho kimebaki.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

 

Leave A Reply