The House of Favourite Newspapers

Flash Back…Ya Mastaa Ndani Ya Skendo Ya Usagaji

0
Jacqueline Wolper

KATIKA ulimwengu wa mastaa wa kike wa kiwanda cha sinema za Kibonngo almaarufu Bongowood, kuna wahusika wake ambao wamewahi kugandwa na skendo nzito ya mapenzi ya jinsi moja yaani usagaji, Ijumaa linakupa flashback. Zipo sababu kadha wa kadha zilizodaiwa kuchangia wao kukumbwa na kashfa hiyo huku ukaribu wenye shaka kati ya staa mmoja na mwingine ukishereheshwa na matendo waliyokuwa wakiyafanya yaliyotafsiriwa kubeba viashiria vya matendo hayo haramu chini ya jua;

WOLPER

Mara kibwena Jacqueline Wolper amekuwa akitajwa kwenye kashfa hiyo. Skendo hiyo ilishika kasi baada ya mwanaume aliyekuwa anatoka naye kipindi cha nyuma aliyetajwa kwa jina maarufu G Model kukiri kuwa, mwandani wake huyo alikuwa na tabia hizo kabla ya kuamua kuiacha.

Wema Sepetu

AUNT NA WEMA

Aunt Ezekiel na Wema Sepetu waliwahi kuwa na ushosti wa kupitiliza uliozaa kashfa hiyo. Katika kipindi cha ushosti wao, walizua viulizo kutokana na kuonekana wakifanyiana mahaba ya ‘mume na mke’, lakini wamekuwa wakipinga kujihusisha na masuala hayo wakidai ni uzungu tu.

 

DAVINA

Halima Yahya ‘Davina’, naye aliwahi kutafunwa na ishu hiyo akidaiwa kufanya kitendo hicho na msanii mwenzake, lakini alikana vikali akiapa kula wala hajui michezo hiyo inachezwaje. Alisema kuwa, alihisi huenda wabaya wake walitaka kumharibia jina.

NISHA

Salma Jabu almaarufu Nisha ni miongoni mwa mastaa wa Bongo Movies waliowahi kutajwa kwenye orodha hiyo. Kama ilivyokuwa kwa wengine, Nisha alitumia nguvu kubwa kujinasua akisema abadani, hawezi kufanya vitendo hivyo na huenda ni watu tu walimtafsiri tofauti kutokana na maneno yake aliyowahi kuongea na kuwafanya wahisi hivyo.

JACK CHUZ & JINI KABULA

Jacqueline Pentzel almaarufu Jack Chuz aliwahi kukumbwa na skendo hiyo akihusishwa mwigizaji mwenzake, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ baada ya picha zao kunaswa wakiwa kwenye mahaba mazito. Hata hivyo, nao walitumia nguvu kubwa kukanusha wakidai kwamba picha hizo zilikuwa za kikazi zaidi na wala hawana michezo hiyo.

VAI WA UKWELI

Mwigizaji Isabela Francis almaarufu Vai wa Ukweli ni miongoni mwa waliowahi kuhusishwa na usagaji, hadi kufikia hatua ya kutengwa na ndugu, jamaa na marafiki. Jambo hilo lilimuumiza mno Vai huku mwenyewe akijitetea kuwa hana tabia hizo, ila kilichomfanya akumbwe na kashfa hiyo ni kutokana na kuwa na marafiki wengi wanaofanya mambo hayo

MADAHA & BELLA B

aby Joseph Madaha na Isabela Mpanda ‘Bella’ wana ukaribu ambao uliwahi kutiliwa shaka kutokana na mapozi ya picha mbalimbali ambazo wamekuwa wakipiga zenye muonekano tata. Wengi wamekuwa wakiwahusisha na vitendo hivyo, japokuwa wamekuwa wakikanusha

MAKALA: MAYASA MARIWATA

 

Leave A Reply