Kartra

Simba Yawafunga Al Merrikh 3-0, Miquissone, Mugalu Watupia

TIMU ya Simba imepata ushindi wa mabao 3-0 leo Machi 16, 2021 dhidi ya Al Merrikh katika Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na unawafanya Simba kufikisha pointi 10 na kuwafanya wasubiri pointi moja tu ili kujihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali.

Kusubili kwa pointi moja kunatokana na mtu wa pili katika kundi A ambaye ni Al Ahly kuwa na pointi saba huku nafasi ya tatu ikishikiliwa na AS Vita wenye pointi nne na Merrikh wakiwa na pointi moja.

Mabao ya Simba yamefungwa na Luís Jose Miquissone 18′, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ 39′ na Chris Mugalu 49′

Kwa maana hiyo zikiwa zimebaki mechi mbili, Simba anahitaji pointi moja tu katika mchezo ujao dhidi ya As Vita na kufikisha pointi 11 akijihakikishia kuongoza kundi A.

Wakati huo Al Ahly wao wakiwa ugenini dhidi ya Al Merrikh hata wakishinda watakuwa na pointi 10 na kuwafanywa washike nafasi ya pili.


⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx


Toa comment