The House of Favourite Newspapers

Fundisho kwa wanaochati, kuwasiliana  na michepuko kwa siri!

0

????????????????????????????????????

Lakini wakati hali ikiwa hivyo, bado wapo ambao wako kwenye uhusiano lakini wamekuwa wakizitumia vibaya simu zao. Unakuta mume wa mtu lakini ana namba za wanawake kibao kwenye simu yake na akiwa mbali na mwenza wake, ni mwendo wa kuchati na kuongea nao mambo yao wanayoyajua.

Vivyo hivyo kwa wanawake, wapo ambao wana wapenzi lakini mawasiliano na vijibwana vya nje yamekuwa yakiendelea kama kawaida.

Hatari zaidi inakuja pale ambapo unagundua kuwa hakuna mwanaume au mwanamke anayeweza kudiriki kumuachia mwenza wake simu yake kwa siku zima.

Achilia mbali kumuachia, hata kuigusa tu ugomvi mkubwa unaweza kuibuka. Kwa nini? Kwa sababu ni watu wachache sana ambao simu zao hazina madhambi.

Sasa leo nataka niwape kisa kimoja ambacho naamini ni fundisho kwa wenye tabia ya kuchati na michepuko wakati wakiwa mbali na wapenzi wao.

Kijana mmoja aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sudi alikuwa na mke wake. Alimpenda sana na kila wakati amekuwa akimwambia hivyo. Mbali na kumwambia mkewe kuwa anampenda pia alimhakikishia kuwa, hata siku moja hatadiriki kumsaliti.

Sudi alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni moja na mkewe alikuwa mfanyabiashara. Kadiri siku zilivyokuwa zinakwenda, Sudi akaanza kubadilika, akawa ni mtu wa kubadili wasichana na mara nyingi amekuwa akiwasiliana nao akiwa mbali na mkewe.

Hata hivyo, Sudi alikuwa na ratiba ya kuwasiliana na michepuko yake siku za Jumatatu hadi Ijumaa, saa tatu asubuhi hadi saa 10.30 jioni, kwani muda huo anakuwa kazini na mkewe anakuwa kwenye pilika zake.

Siku moja ya Jumanne saa sita mchana wakati Sudi akiwa kazini alianguka ghafla. Akachukuliwa na kukimbizwa hospitalini na mkewe akapigiwa simu kupewa taarifa.

Mke akafika haraka na kumkuta mumewe hajitambui. Wakati jitihada za kumtibu zikiendelea, mke akaomba apewe simu ya mumewe ili afanye mawasiliano.

Wakati mke akichukua ile simu, kumbe mume alishaanza kuwasiliana na michepuko yake. Hee! Mara meseji ikaingia kwenye simu ya mume kutoka kwa mtu aliyeseviwa Fundi 1. Meseji yenyewe iliandikwa hivi: Baby jana usiku nilitamani nikupigie, nikajua utakuwa kwa mkeo. Naomba basi ile pesa ya pango maana mwenye nyumba ananisumbua sana.” Mke akapigwa butwaa.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

globalbreakingnews.JPG

Mara ikaingia nyingine kutoka kwa mtu aliyeseviwa jina la Fundi 3, iliandikwa hivi: “Siwezi kukuacha, nakupenda kuliko unavyofikiria.” Kimsingi ziliingia meseji nyingi ambazo zilimchanganya mkewe. Alipojaribu kuingia inbox na out box akakuta meseji nzito zilizomfanya yule mama aanguke na kuzimia.

Likawa ni tatizo lingine! Baada ya kupita muda mfupi, mume akazinduka na kuambiwa kilichompata. Akashangaa sana lakini akaambiwa na mkewe naye alifika pale na katika mazingira ya kushangaza alianguka.

Mume aliposikia hivyo, akakurupuka na kwenda alipokuwa amelala mkewe na kuchukua simu yake. Kuangalia akakuta meseji kibao kutoka kwa michepuko yake na zilikuwa zimesomwa na mkewe.

Mume akajua kimenuka! Mke alipozinduka mume akamuomba msamaha sana na alipokubaliwa, sasa kabadilika na ameachana na michepuko. Wewe unayechati na michepuko ukiwa mbali na mwenza wako umejifunza kitu? Tuwasiliane kwa namba hizo hapo juu.

Leave A Reply