The House of Favourite Newspapers

Gigy Akiri Kuchoropoa Mimba 3

Gigy Money (Kushoto) na rafiki yake Lily

STORI: WAANDISHI WETU | AMANI | HABARI

MWANADADA ambaye ni video queen na mtangazaji wa kituo kimoja cha redio Bongo, Kituo cha Redio cha Choice FM, Gift Stanford ‘Gigy Money’ hivi karibuni alinasa kwenye mtego wa Kite   ngo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM), cha Global Publishers na kufunguka kuwa mpaka sasa amekwisha choropoa ujauzito wa wanaume watatu.

Gigy alinasa kwenye mtego huo baada ya kutafutwa na kachero wa OFM ambaye alimuomba kukutana naye kwa ajili ya mazungumzo ya kimuziki, baada ya kukutana maeneo ya Mlimani City na kuanza mazungumzo, mwanadada huyo alianza kufunguka mambo yake mengine ya siri ikiwa ni pamoja na kutoa kila ujauzito anaoupata.MAONGEZI YALIKUWA HIVI

Gigy Money akiwa na Idris Sultan
Gigy Money katika pozi

OFM: Gharama ya kufanya kazi na wewe inaonekana kuwa juu sana eeeh?

Gigy: Ndiyo, mimi nina jina kubwa na watu wengi wananifahamu, sasa inabidi kuishi kulingana na jina langu maana sitaki kulishusha na ninahitaji kufanya lolote lile ili tu kuwa staa mkubwa.

OFM: Unaposema lolote lile unamaanisha nini?

Gigy: Namaanisha lolote lile, kwani wewe hufahamu maana
ya lolote lile?

OFM: Nafahamu, lakini sijajua ni kama kipi?

Gigy: Kama kuzaa. Siwezi kuzaa kwa sasa hata kwa dawa.

OFM: Ina maana mpaka sasa hujawahi kunasa ujauzito? Gigy:

Nishanasa tena kama mara tatu hivi, lakini kila ninaponasa natoa, na hata kama nikinasa hata leo nitatoa, kwa sababu nikizaa siwezi kufikia malengo yangu ya kuwa staa. Lakini pia ninaangalia mtu wa kuzaa naye, siwezi kuzaa na mtu yeyote yule.

AMEWAHI KUFANYA KAZI BAA

Baada ya mazungumzo yake juu ya kuchoropoa ujauzito
mara tatu kufikia tamati huku akikataa kuwataja waliomjaza ujauzito huo, mwanadada huyo alizidi kumwaga ubuyu mbele ya OFM kuwa ameshawahi kufanya kazi baa muda mrefu kwa sababu mama yake anamiliki baa.

“Mimi hawa wahudumu wa humu hata hawanitishi, unajua nimewahi kufanya kazi baa, nimehudumia sana, nafahamu kila kitu kuhusu huduma, kwa hiyo hata hawa wahudumu wa hapa hawanitishi,” alisema Gigy.


AKIRI AMEJAWA NA UTOTO KICHWANI

Katika hali ya kushangaza, mwanadada huyo alizidi kufunguka mambo mengine mengi mbele ya paparazi wetu ikiwemo juu ya mambo anayokuwa anafanya mitandaoni, na kuonekana mkorofi.
Juu ya suala la ukorofi alikiri kweli yeye ni mkorofi, lakini akaongeza kuwa anafanya hivyo kwa sababu amejawa na akili ya utoto kichwani mwake maana bado ana umri mdogo.

“Unajua mimi bado mtoto, kwa hiyo unaweza kushangazwa na baadhi ya mambo ambayo nayafanya, lakini huo wote ni utoto, mimi umri wangu bado mdogo!” alisema video queen huyo.

AKATAA KUENDELEA KUZUNGUMZIA MAMBO YAKE

Hata hivyo baada ya mazungumzo hayo na mengine mengi binafsi aliyofunguka mbele ya OFM,Gigy alikataa kuendelea kuzungumzia habari hizo alizokuwa anachimbwa na kachero wa OFM, badala yake alitaka maongezi yao yabadilike na kuzungumzia kazi iliyokuwa imewakutanisha mahali hapo.

Save

Save

Comments are closed.