The House of Favourite Newspapers

Gigy: Barakah Kanikimbiza na Panga

0

Ugomvi wa King Kiba na Shilole umeonekana kuendelea kupita na wengi na raundi hii umehamia kwa Barakah The Prince na Gigy Money.

Hii imetokana na Insta Live ya Gigy Money baada ya kumwambia King Kiba kuwa kipaji bila nidhamu atakuwa kama Barakah.

Barakah alitumia ukurasa wake wa Instagram kumchana Gigy Money kwa alichokifanya huku akitumia kauli nyingi za dharau na kuambatanisha picha zake za nusu utupu.

Kwa upande wa Gigy Money hakulaza damu, akaibuka na ku-comment akimuahidi Barakah kuwa atamtolea ma-file yake maana anamjua nje ndani.

Kupitia Insta Live, Gigy amemchana Barakah ile mbaya akikumbushia tukio lake la kumkimbiza na panga.

Gigy anasema kwa sasa Barakah ameishiwa na nyimbo na sasa anachambana na wanawake.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply