The House of Favourite Newspapers

Gigy Money Aandikiwa Barua BASATA

0

KATIBU Mkuu wa Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya Tanzania Samwel Mbwana ‘Braton’ amesema wamewaandikia barua Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhusu kuachiwa kwa msanii Gigy Money.

 

“Suala la Gigy Money lipo wazi na lipo mikononi mwa BASATA, tulishapeleka barua na tumewaomba pia tunategemea kesho Mei 8, Mhe Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo atalitolea tamko.”

 

“Jinsi alivyokuwa amefungiwa walikuwa wamefungiwa watu wawili kwa kesi moja, lakini mwingine ameachiwa ameenda halafu yeye bado anatumikia kifungo, ni kitu ambacho kinaatuumiza, tumewaandikia barua,” Samwel Mbwana ‘Braton’.

 

Siku ya Januari 5 msaniii Gigy Money alitolewa hukumu na BASATA ya kutojihusisha na masuala ya sanaa kwa muda wa miezi 6 na faini ya Tsh Milioni 1 kwa kosa la ukiukwaji wa maadili.

Leave A Reply