The House of Favourite Newspapers

Gilla anusurika kufa maji

0

Gilla (2)Gilla akiogelea
Gilla (1)
…akiokolewa baada ya kuzidiwa na maji.Gilla (5)…akipatiwa huduma ya kwanza
Gilla (6)
Gilla-(10)
Stori:Mayasa Mariwata

MSANII wa filamu Bongo, Glasnost Kalinga ‘Gilla’ amejikuta akinusurika kifo wakati alipokuwa akiogelea kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar baada ya maji kumzidi kiwango na kuokolewa na wasamaria wema juzi Alhamisi wakati watu wakiwa katika harakati za kuusubiria Mwaka Mpya.

Gilla-(4)Kwa mujibu wa chanzo chetu, awali msanii huyo ambaye alifika mahali hapo mida ya jioni aliamua kutulia kwenye viti vilivyokuwa katika baa moja ufukweni hapo lakini baada ya kupandwa na mzuka wa kuogelea majira ya saa 12 jioni, ndipo alipoamua kuvua nguo na kujitosa majini.

Gilla (7)“Nakwambia yule msanii chupuchupu afe, ilikuwa bahati sana kupona mana’ke muda ule maji yalikuwa mengi sana, tulinza kuona mtu anatapatapa akitafuta njia ya kujiokoa huku maji yakionekana kumzidi nguvu, ndipo watu wakazama majini na kumsaidia,” kilisema chanzo chetu na kutuma picha za tukio ofisini.

Baada ya kupewa taarifa hiyo, paparazi wetu alimvutia waya Gilla na kufunguka kuwa:
“Sijui leo familia yangu ingeongea nini ingebaki stori tu, tatizo ni kwamba nilijiona mimi ni bingwa wa kuogelea, mzuka uliponipanda, nikaelekea baharini kuoga kwa manjonjo ila maji yalipoongezeka, nikaanza kuzidiwa hivyo kutapatapa kama njia ya kutafuta msaada. Gilla (9)Gilla-(14)…baada ya kuzinduka

Nawashukuu walioniokoa,” alisema Gilla.

Leave A Reply