The House of Favourite Newspapers

Global FC kuichakaza TSJ kesho

KIKOSI ghali zaidi ndani ya Sinza, Global FC kimetangaza kuichakaza timu ya Chuo cha Uandishi wa Habari cha Times “TSJ” zitakapokutana katika mchezo wa kirafi ki utakaochezwa kesho Ijumaa kwenye Uwanja wa St Mary’s, Tabata jijini Dar.

 

Matajiri hao walio chini ya udhamini wa Ashish Cinematographer, watautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi ya ndani ya Global Group kati ya Waliooa FC na Wasiooa FC itakayofanyika Septemba 6, mwaka huu.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nahodha wa Global FC, Wilbert Molandi ambaye aliwahi kusoma TSJ, alisema mchezo huo una lengo la kufundishana baadhi ya vitu na wanafunzi hao.

 

“Tunacheza na wadogo zetu ambao wanasomea uandishi wa habari, hivyo mechi hii ni sehemu ya kufundishana na wanafunzi hao maana hata mimi nimewahi kusoma hapo,” alisema Molandi ambaye huenda akawa miongoni mwa mastaa wa Global watakaong’ara kwenye Ligi Daraja la Pili msimu huu.

MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI SARAH MSAFIRI NDANI YA +255 GLOBAL RADIO

Comments are closed.