The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI AUG 19: MAGARI YATEKETEA KWA MOTO KAGERA

MAGARI kadhaa yameteketea kwa moto leo baada ya lori la mafuta la kampuni ya Ratco kufeli breki na kugonga magari mengine kumi yaliyokuwa yanapakia pumba katika eneo la Rusumo mkoani Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Olomi, amethibitisha tukio hilo na amesema wanaendelea na jitihada za kuuzima moto huo uliokuwa unaendelea hadi mchana ambao ulioanza saa tatu asubuhi baada ya magari mawili kugongana eneo hilo wilayani Ngara.

Comments are closed.