The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI FEBR 21: KIMENUKA! Prof LIPUMBA Amvaa MAALIM SEIF! – VIDEO

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba amemtaka Katibu mkuu wa chama hicho maalim Seif Hamad kutochukua hatua yoyote ya kujitoa katika chama mpaka kamati kuu ya chama itakapo kaa kumjadili. Akizungumza na waandishi wa habari Prof Lipumba ameyasema hayo baada ya Mahakama Kuu kuifuta Bodi iliyokuwa imeundwa na katibu wa chama hicho Maalim Seif.

Aidha prof Lipumba amesema tofauti yake kisiasa na Katibu wake ni baada ya kuikataa hoja yake yakutaka kuwa na muungano wa mkataba ndani ya chama utakaotengeneza serikali mbili.

Hivi karibuni mahakama kuu ilitengua uteuzi wa wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Wananchi CUF wa kambi ya mwenyekiti anayetambuliwa na ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa Prof Ibrahim Lipumba.

Uamuzi huo ulitolewa Februari 18 mwaka huu siku ya jumatatu na jaji Dakt Benhajj Masoud baada ya kubatilisha uteuzi wao. Mwenyekiti wa chama hicho Prof Ibrahimu Lipumba na Katibu mkuu wa Chama Maalim Seif Hamad wamekuwa kwenye mvutano wa muda mrefu ndani ya chama hicho.

Comments are closed.