The House of Favourite Newspapers

GLOBAL HABARI JAN 30: LUGOLA Anyanyuliwa BUNGENI, Sakata la Mauaji Njombe – VIDEO

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amesema serikali kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama nchini imeshaanza kushughulikia mauaji ya watoto yanayoendelea mkoani Njombe, huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina.

Waziri Lugola ameyasema hayo wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa Mufindi Kusini (CCM), Mendrad Kigola Akihoji ni mkakati gani uliowekwa na Serikali kukomesha mauaji ya watoto mkoani Njombe ili kurejesha amani mkoani humo.

Pia Lugola amewaomba wabunge wa mkoa huo kutoa ushirikiano kwa serikali ili kuweza kutokomeza ukatili huo unaoendelea dhidi ya watoto.

Januari 29 mwaka huu Jeshi la Polisi Mkoani Njombe limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wa mkoa huo waliozua tafrani kwa kuandamana barabarani baada ya wakazi hao kumkamata mtu mmoja aliyesadikiwa kuwa ni muhusika wa matukio ya utekaji watoto Mkoani humo.

Comments are closed.