The House of Favourite Newspapers

Global Habari Juni 23 – Rais Samia Ashiriki Mkutano wa SADC

0

Leo June 23,2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika Mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Joaquim Chissano uliopo Maputo Nchini Msumbiji.

 

Rais Samia aliondoka Nchini jana June 22,2021 na atakuwa na ziara ya kikazi ya siku 2 Nchini Humo ambapo lengo kuu la Mkutano huo wa Dharura wa Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika SADC ni kujadili mambo mbalimbali ya kiuchumi, kibiashara na mabadiliko ya Tabia ya Nchi

Leave A Reply