The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Global TV Kenya Yamuibua Juacali

0
Msanii Juacali.

 

Paul Julius Nunda, maarufu kwa jina la Juacali, Msanii wa muziki wa Genge kutoka nchini Kenya ameongea na Global TV Kenya kuhusu gemu ya muziki. Amefunguka namna ambavyo mwaka jana ulikuwa mzuri kwake kwani aligonga shoo za kutosha na kuwa kivutio kikubwa cha mademu, hasa kutokana na wimbo wake maarufu wa NGELI YA GENGE.

 

Mwaka huu pia JUACALI, ambaye yuko chini ya Producer Clemo, anatarajia kuibuka na ngoma nyingine mbili mara tu baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 28.

 

Katika mazungumzo haya na Global TV Online kutoka Kenya, Juacali anazungumza kinyonge kama mtu anayeumwa au ambaye ana tatizo fulani.

Hebu msikilize mwenyewe.

 

Leave A Reply