The House of Favourite Newspapers

Mzee Mwinyi Awavunja Watu Mbavu – Video

0

Ni zaidi ya wiki moja sasa tangu Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipotangaza kuwa Hayati Rais John Pombe Magufuli amefariki dunia.

 

 

Na hapo jana kiongozi huyo aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipumzishwa katika nyumba yake ya milele huku huzuni, simanzi na majonzi vikitanda kote nchini humo.

 

Watu wa tabaka mbalimbali walipata fusra ya kuzungumza wakati wa kumuaga Rais John Pombe Magufuli miongoni mwao akiwa ni Rais Mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi katika hotuba iliyowaacha wengi wakitabasamu.

 

Waombolezaji wamejikuta wakiangua vicheko kutokana na maneno ya Mzee Mwinyi hasa baada ya kusahau majina ya watoto wake wa kuzaa na kusahau kuwa pale alipokuwa ni Chato.

 

SIKILIZA HOTUBA YAKE ALIVYOWACHEKESHA WATU

Leave A Reply