Gomes: Tunakwenda Kigoma Kulipa Kisasi

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amewataadharisha wapinzani wao wa jadi, Yanga kujipanga vizuri, kwani wanakwenda Kigoma kulipa kisasi cha kufungwa Julai 3, mwaka huu.

 

Julai 25, mwaka huu, Yanga na Simba zinatarajiwa kupambana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam utakaochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

 

Simba ina kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa mwisho kwa bao 1-0 dhidi ya Yanga uliochezwa Julai 3, mwaka huu Uwanja wa Mkapa, Dar ukiwa ni wa Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spoti Xtra, kuhusu fainali hiyo, Gomes alisema: “Tulipoteza mchezo wa Julai 3 hapa Dar es Salaam, ni matokeo ambayo yalituumiza sana sisi pamoja na mashabiki wetu, hivyo tunakwenda Kigoma tukijua tunakwenda kwenye mchezo wa kisasi.

 

“Tumerekebisha makosa ambayo tuliyafanya kwenye mchezo uliopita hasa kwa namna ya kuanza mchezo, lakini pia tumeongeza baadhi ya vitu, malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda ubingwa wa FA.”

STORI: JOEL THOMAS ,Dar es Salaam

 


Toa comment