The House of Favourite Newspapers

Gomez Avunja Rekodi ya Beyonce Katika Instagram kwa Picha Yake

Tokeo la picha la Selena Gomez Breaks Beyonce's Instagram Record With This Photo

MWIMBAJI na mwigizaji wa Marekani, Selena Gomez, alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake juzi (Jumatatu) kwa kuvunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na mwanamuziki, Beyonce.

Alivunja rekodi hiyo alipoweka picha yake (juu) akiwa na  gauni lisilokuwa na mabega kwenye mtandao wa Instagram na kupata ‘likes’ milioni moja katika muda wa dakika 13 tu, chini ya rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Beyonce.

Hadi sasa, Selena amepata ‘likes’ milioni 8.4 kwa picha hiyo na idadi inaongezeka.  Beyonce alikuwa anashikilia rekodi hiyo alipotanza ujauzito wake na alipoweka picha za watoto wake mapacha, ambapo alipata likes milioni 116.5 tangu alipo-posti vitu hivyo.Tokeo la picha la Selena Gomez Breaks Beyonce's Instagram Record With This Photo

Kwa mujibu wa  Billboard,  picha hizo za mapacha wa Beyonce alizotoa zaidi ya mwaka mmoja uliopita, zilipata ‘likes’ milioni  7.8 katika muda wa saa 12 wakati ambapo ujauzito wake ulipotangazwa ulipata ‘likes’ milioni  6.4 katika saa za mwanzo.

Comments are closed.