The House of Favourite Newspapers

GSM Yaendelea Kugawa Zawadi za Sikukuu Kwa Wateja Wake

0
Kaimu Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM, Smart Deus (katikati) akizungumza wakati wa uchezeshaji wa droo hiyo. Kushoto ni Meneja Biashara wa GSM Home, Fahad Mohammed na kulia ni Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Michael.

MADUKA ya GSM imeendelea kugawa zawadi za sikukuu kwa wateja wake katika promosheni ya Shinda Ungarishe Nyumba yako iliyokuwa ikiendeshwa kwenye maduka hayo kwa ajili ya kuwazawadia wateja wake. Katika droo ya pili ya promosheni hiyo iliyochezeshwa duka la GSM Home lililopo Mikocheni jijini Dar, Baraka Kimaro mkazi wa jijini Dar aliibuka mshindi na wa zawadi ya picha kubwa ya kupamba ukuta (Art Wall). Akizungumza baada ya kupatikana mshindi huyo, Kaimu Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM, Smart Deus amempongeza mteja huyo na kuwataka wengine waendelee kushiriki kwenye promosheni hiyo. Droo hiyo ilichezeshwa mbele ya wanahabari chini ya usimamizi wa mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Pendo Michael.

Smart Deus akilisoma jina la mshindi baada ya kupatikana.
Zawadi ya mshindi ikioneshwa ambayo mwenyewe anasubiriwa kwenda kuichukua.  
Leave A Reply