The House of Favourite Newspapers

GSM Yazindua Tokomeza Godoro Bovu

 

Meneja bidhaa wa GSM Tanzania,Ismael Kassim(kushoto)pamoja na Meneja wa kitengo cha Fedha wa kampuni hiyo,Karim Kassingo(kulia)wakimsikiliza Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na waandishi wa habari jijini Dares Salaam(hawapo pichani)wakati wa Uzinduzi wa kampeni ya TOKOMEZA GODORO BOVU TUMIA GODORO CHAPA GSM.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group,Matina Nkurlu (katikati) akionesha msisitizo wa jambo.
Meneja bidhaa wa GSM Tanzania,Ismael Kassim(kushoto)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya ubora wa magodoro chapa GSM wakati wa Uzinduzi wa kampeni hiyo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiongozwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group,Matina Nkurlu(watatu kushoto)kutembelea kiwanda cha kuzalisha magodoro cha kampuni hiyo.

 

 

 

KAMPUNI ya GSM Tanzania, imezindua kampeni kabambe itakayofanyika nchi nzima inayofahamika kama”Tokomeza Godoro Bovu tumia godoro chapa GSM” ikilenga kutaka watanzania wanufaike na matunda ya
viwanda vya ndani ya nchi yao na kuhamasisha utumiaji wa magodoro Chapa GSM yenye ubora wa hali ya juu na yanayodumu kwa muda mrefu,Pia yanayouzwa kwa bei nzuri ambayo kila mtanzania anaimudu.

 

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa GSM Group, Matina Nkurlu, alisema kuwa kampeni hiyo itakuwa kwa awamu tofauti, awamu ya kwanza ikianzia mikoa ya
Pwani, Lindi na Mtwara.

 

Alisema wameona ni vema kutambulisha kwa jamii ya watanzania magodoro hayo baada ya kubaini wengi wao wamekuwa wakinunua bidhaa za magodoro zisizo na ubora wa kimataifa na matokeo yake inakuwa ni
hasara na mzigo kwao badala ya kuwasaidia.

 

“Kuna magodoro ambayo unaweza kununua kwa kiasi kikubwa cha fedha lakini yasidumu kwa muda mrefu, hii ni sababu mojawapo ya kuongeza umasikini kwa Watanzania kwa kuwafanya kila mara kununua magodoro
mapya.

“Kwa kutambua hilo, tumeona ni vema tukawaletea watanzania wenzetu magodoro imara yenye ubora wa kimataifa na ya kisasa kabisa yaliyodhibitishwa na TBS, ni magodoro HD na Spring yenye uwezo wa kusafishika kiurahisi na kunyonya kila aina ya majimaji na kuwa makavu wakati wote.

 

 

“Ukinunua godoro chapa GSM, hutajutia fedha zako kamwe.  Kazi kwenu wana Mtwara na Lindi, kwani tunawaletea magodoro kwa bei yenu nyie muitakayo ninyi hususan kwa mwezi huu wa kumi, kampeni hii  inaanzia leo tarehe 17 Lindi na kuelekea Mtwara Mjini ambapo tutapita kila Kijiji na tamati itakuwa tarehe 27, Nachingwea Mjini ambapo kutakuwa na tamasha kubwa la michezo pia,” alisema Nkurlu.

 

Alisisitiza kwamba kutakuwa na bei za jumla kwa wafanyabiashara au mawakala na bei za rejareja kwa watu wote na kwamba baada ya uzinduzi wa bidhaa yao hiyo katika maeneo tajwa hapo juu, watahamia mikoa mingine na hivyo kuwataka Watanzania kutofanya kosa kwa kununua magodoro mengine zaidi ya yale yanayozalishwa na kampuni yao ya GSM Tanzania kwani ni magodoro bora na ya bei nzuri kwa kila Mtanzania.

 

Ikumbukwe pia Magodoro ya GSM ni moja ya wadhamini wakuu wa club kubwa ya mpira hapa nchini Yanga Afrikani Club. Lengo la GSM ni kuhakikisha kuwa kila mtanzania analala kwenye godoro lenye ubora wa
hali ya juu kwa-ajili ya kuanza kesho yake.

 

GSM Tanzania imekuwa ikijihusisha na utengenezaji na usambazaji wa bidhaa mbalimbali za nyumbani na ujenzi zenye ubora wa hali ya juu kama mabati, misumari, Hamira na bidhaa nyingi mbalimbali.

Comments are closed.