The House of Favourite Newspapers

Gwajima: Nchi ni Lazima Iwe na Maono ya Miaka Mingi – Video

0

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, amesema kwa sasa Tanzania haina maono ya muda mrefu kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi bali kuna Ilani za Vyama na mipango ya muda mfupi.

 

Amefafanua kuwepo kwa maono ya muda mrefu kutasaidia hata kumpima Rais anapoingia Madarakani kwa namna ambavyo anayatekeleza maono yaliyowekwa ila kwasasa tunaona tunasogea lakini ni kwa maono ya kila Serikali mpya inapoingia Madarakani.

 

Ameongeza “Sasa hivi hatuna Vision bali tuna mambo ya kukimbiza. Kila Mwaka tunatafuta Madawati, kwani hakuna tawimu za kuonesha Mwaka huu tunahitaji Madawati mangapi kutokana na idadi ya Wanafunzi?”.

 

Amesema hayo wakati akichangia mapendekezo yake katika makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Leave A Reply