The House of Favourite Newspapers

H-Baba Atahadharishwa Kumzeesha Flora

0

h-baba-na-floraH-Baba, mkewe Flora Mvungi na mtoto wao.

Stori: Hamida Hassan

Licha ya H-Baba kudai kuwa, mkewe Flora Mvungi anazidi kuwa mzuri licha ya kuwa mama wa watoto wawili, mashabiki wake wamemtahadharisha kwa kumwambia kuwa, asipoangalia atamzeesha bila kutarajia.

Flora juzikati alidaiwa kujifungua mtoto wa tatu na alipotupia mtandaoni picha inayomuonesha akiwa na baby, wengi walimpongeza lakini wapo waliompa H-Baba tahadhari kuwa, anavyombebesha mimba za fasta mkewe atakuwa anamfanya aonekane mmama wakati bado ni binti.

“Unajua bwana kila mtu ana uamuzi wake, kitendo cha H- Baba kutaka kupata watoto fasta, siyo kibaya lakini Flora anazeeka yule, muoneni hivi hivi…” alisema mdau mmoja.

H- Baba sasa ana watoto watatu ambao ni Tanzania, Afrika na huyo mdogo ambaye taarifa zake hazijaanikwa.

Leave A Reply