The House of Favourite Newspapers

Hafla Ya Uzinduzi wa Mauzo ya Hisa za Upendeleo za Kampuni ya TCCIA Investment Plc Yafaana!

0
Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), CPA Nicodemus Mkama akizungumza jambo katika hafla hiyo.

Serikali kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ina jukumu la kuweka mazingira wezeshi ya kisera, kisheria na kiutendaji ili kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha za kugharamia shughuli za maendeleo.

Kadiri Taifa letu linavyosonga mbele katika utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 yaani the Third National Five-Year Development Plan (FYDP III) wenye dhima ya kujenga “Uchumi Shindani kwa Maendeleo ya Watu”, mahitaji ya rasilimali fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo na miundombinu yanaongezeka. Ili kufanikisha azma hii, kunahitajika uwepo wa bidhaa bunifu ambazo zinaleta anuwai katika masoko ya fedha, ikiwa ni pamoja na hisa za upendeleo kama hizi za TCCIA Investment Plc. Aidha, uwepo wa bidhaa nyingi katika masoko ya mitaji unachangia utekelezaji wa Sera za Fedha (Monetary policy) katika Uchumi na Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi (economic empowerment policy); kuongezeka kwa akiba

3

hapa nchini; kupanuka kwa uwekezaji unaoleta ongezeko la ajira; Mapato kwa njia ya kodi kwa Serikali na kuinua kipato cha watanzania kwa ujumla.

Ndugu Wageni Waalikwa, Mnamo tarehe 3 Novemba 2023, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) iliidhinisha Waraka wa Matarajio wa TCCIA Investment Plc kuuza hisa za upendeleo 72,957,660 kwa wanahisa wake kwa bei ya Shilingi 145 kwa kila hisa katika uwiano wa hisa moja mpya kwa kila hisa moja aliyonayo mwekezaji kwa sasa. Idhini imetolewa na CMSA baada ya TCCIA Investment Plc kukidhi matakwa ya Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Sura ya 79 ya Sheria za Tanzania; na Miongozo ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya Utoaji wa Hisa za Upendeleo yaani “Capital Markets and Securities (The Capitalisation and Right
Issues), Regulations 2000”. Kwa mantiki hii mauzo ya hisa za upendeleo za TCCIA Investment Plc yamekidhi matakwa ya Sheria, Kanuni na Miongozo ya Masoko ya Mitaji.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCCIA Investment Plc; Dkt. Fortunatus Magambo,  

Ndugu Wageni Waalikwa, Mchakato wa kuidhinisha mauzo ya hisa unahusisha taasisi na wataalam mbalimbali ikiwa ni pamoja na: Mshauri kiongozi na Dalali Mfadhili wa TCCIA Investment Plc, iTrust Finance Limited; Mshauri wa Sheria, Endoxa Law; Mkaguzi na Mtoa Taarifa za Hesabu, Auditax International. Ninatambua kwamba, kazi hiyo haikuwa ndogo na rahisi lakini mmeweza kufanya kazi yenu vizuri na kufanikisha hatua hii kwa weledi na kwa ufanisi mkubwa, na hivyo kupata idhini kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA). Hongereni sana!! Aidha, pongezi kubwa

4

zinakwenda kwa Bodi na uongozi wa TCCIA Investment Plc kwa kufanya uamuzi wa mchakato huu. Hongereni sana!!.

Ndugu Wageni Waalikwa, Mauzo ya hisa za upendeleo za TCCIA Investment Plc kwenye soko la awali yanafunguliwa leo hii tarehe 16 Novemba 2023 na yanatarajiwa kufungwa tarehe 1 Desemba 2023, ambapo TCCIA Investment Plc inatarajia kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni 10.58.
Fedha zitakazopatikana kupitia mauzo haya zitaiwezesha TCCIA Investment Plc kukuza uwekezaji wake katika dhamana mbalimbali za masoko ya mitaji, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika hisa za kampuni, hatifungani na vipande katika mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC).

Hii itawezesha kampuni kutimiza malengo yake ya kimkakati ya kukuza thamani ya uwekezaji wa wanahisa katika kampuni.

Ndugu Wageni Waalikwa, Masoko ya mitaji huchochea maendeleo ya uchumi kwa kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha na kuimarisha utawala bora na hivyo kuleta tija kwa kampuni na taasisi. Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) itaendelea kujenga mazingira wezeshi na shirikishi ili kuwezesha taasisi katika sekta ya umma na binafsi kutumia masoko ya mitaji kupata fedha za kutekeleza miradi na shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuuza hisa kwa umma (equity financing); hatifungani za miundombinu (infrastructure bonds); hatifungani rafiki wa mazingira (green bonds); hatifungani za bluu (blue bonds); hatifungani za jamii (social bonds); na hatifungani za taasisi za Serikali (subnational bonds).

5

Ndugu Wageni Waalikwa, Napenda kuhitimisha kwa kutoa rai kwa kampuni na taasisi katika sekta binafsi na umma kutumia fursa katika masoko ya mitaji kupata fedha za kugharamia shughuli za kibiashara na miradi ya maendeleo. Hatua hii ni muhimu kwa ustawi wa kampuni, ukuaji wa sekta ya fedha na ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Leave A Reply